mneteblogsport
Tuesday, July 21, 2015
Nkurunziza anatarajiwa kushinda
Raia wa Burundi wanapiga kura Jumanne hii katika zoezi lililoghubikwa na milio ya risasi na miripuko ya magruneti, huku rais Pierre Nkurunziza akitazamiwa kushinda muhula wa tatu licha ya ukosoaji wa kimataifa.
PICHAZ: HAWA NDIO MASTAA WAKUBWA WA NIGERIA WALIOFUNGA NDOA ZA KIFAHARI DUNIAN 2015
JAPOKUWA mwaka huu wa 2015 umepita nusu yake ni mengi yametokea katika ulimwengu wa burudani ambapo waburudishaji wengi walioanza mwaka wakiwa ‘wapweke’ hivi sasa wana wenza wao waliofunga nao ndoa na wanategemea kufanya hivyo kabla mwaka huu haujaisha.
Mtandao wa Nigeriafilms.com umekuwa ukiweka kumbukumbu na sasa unaweza kuonyesha ndoa za ‘nguvu’ ambazo zimetamba katika nusu ya kwanza ya mwaka 2015.
Ndoa ya kimila iliwakutanisha Peter, mmoja wa mapacha wa kundi la muziki la Psquare alipomchukua mpenzi wake wa siku nyingi na mama wa mtoto wake, , Anita Isama. Tukio hilo lilifanyika mwezi Januari huko Ikoyi, Nigeria
Kama ilivyokuwa kwa kaka yake, mwanamuzaiki maarufu, Peter Okoye, na mama wa watoto wake wawili, Lola Omotayo, waliimarisha uhusiano wao kwa kufunga ndoa huko Ikoyi.
Wawili hawa walioana siku ya Wapendanao ya Valentine -- Februari 14 – katika ndoa ya kimyakimpya jijini Accra, Ghana ambapo biharusi Damilola Adegbite alikutana na mpenzi wake, mtoto wa mfalme wa kikabila huko Ghana, Chris Attoh, kwenye mahojiano ya kipindi cha televisheni cha Mnet cha Tinsel.
Japokuwa wawili hao wanasema watafunga ndoa nchini Nigeria, marafiki zao wanasema wana hamu ya kuona hilo linatokea kabla ya kumalizika kwa mwaka 2015.
NI dhahiri Gbenro Ajibade bado ana furaha isiyomithilika kwa kumuoa kipenzi chake, Osas Ighodaro, ambaye hadi sasa bado wako kwenye fungate. Wawili hao walioana Jumamosi ya Julai 4, 2015 jijini New York Marekani.:
Mtandao wa Nigeriafilms.com umekuwa ukiweka kumbukumbu na sasa unaweza kuonyesha ndoa za ‘nguvu’ ambazo zimetamba katika nusu ya kwanza ya mwaka 2015.
![]() |
Paul Okoye na AnitaIsama . |
![]() |
Peter Okoye na Lola Omotayo-Okoye. |
![]() |
Chris Attoh na Damilola Adegbite. |
Japokuwa wawili hao wanasema watafunga ndoa nchini Nigeria, marafiki zao wanasema wana hamu ya kuona hilo linatokea kabla ya kumalizika kwa mwaka 2015.
![]() |
Gbenro Ajibade na Osas Ighodaro. |
Kenyatta: Hatutajadili jinsia moja
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa maswala la mapenzi ya jinsia moja hayajaratibiwa katika mazungumzo baina yake na mgeni wake mashuhuri rais wa Marekani Barack Obama.
Rais Kenyatta aliyasema hayo katika hotuba kwa waandishi wa habari kuhusu ratiba ya rais Obama nchini humo.
Kenyatta alisema kuwa yeye anatarajia kumpokea rais Obama siku ya ijumaa na kuwa
''Kama wakenya tiaf letu linakabiliwa na changamoto nyingi tu nafikiri tunamaswala ya muhumi zaidi ya kujadiliwa mbali na hilo la mapenzi ya jinsia moja'' alisema rais Kenyatta akijibu swali alilorushiwa na mwanahabari.
Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Kenya.

''Hii ni fursa nzuri na kubwa kwa wajasiria mali wakenya kukutana na kubadilishana mawazo na wenzao wa kimataifa'' alisema Kenyatta.
Vijana wetu bila shaka wameweka kigezo cha ubora katika ujasiria mali na ubunifu hata kuvutia mabwenyenye wa kimataifa wanaotafuta sekta za kuwekeza''aliongezea bwana Uhuru.
Mbali na hayo bwana Kenyatta alikariri kuwa Obama atakuwa mgeni wa serikali ya Kenya wala sio yeye kama rais Uhuru Kenyatta.
Aidha alisema ''swala la iwapo atakutana na naibu wa rais bwana William Ruto licha ya kukabiliwa na mashtaka katika mahakama ya ICC huko Hague halipaswi kuibuka''.
Huku hayo yakijiri, hali ya usalama imeimarishwa vilivyo katika mji wa Nairobi na viunga vyake na hasala maeneo yanayotarajiwa kuwa mwenyeji wa rais Obama.
Helikopta 4 za kijeshi za Marekani zilipaa juu ya mji wa Nairobi na kisha kutua katika chuo kikuu cha Kenyatta lililoko viungani mwa jiji hilo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo lake
Waziri mkuu Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo lake la uchaguzi la Katavi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo.Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wengine nafasi.
Ziara ya mfalme wa Saudia Ufaransa yazua Ubishi
Ubishi umeibuka nchini Ufaransa, baada ya ufukwe maarufu wa bahari wa Riviera kufungwa ilikumruhusu mfalme wa Saudi Arabia na familia yake kujivinjari kwa amani faraghani.
Viongozi wa mji wa Vallauriswametangaza kuwa watafunga sehemu kubwa ya ufukwe huo ilikuhakikisha usalama wa mfalme huyo familia yake na takriban ujumbe wa watu 400.
Familia hiyo ya kifalme, inatarajiwa kuishi katika jumba la kifahari lililoko huko.
Jumba hilo lililowahi wakati mmoja kuwa jumba la mapumziko la Sir Winston Churchill linatarajiwa kuzingirwa na maafisa wa usalama.
Maafisa wa Vallauris iliyoko kwenye mwambao wa Cote d'Azur, kilomita 10 kutoka kwenye ufukwe huo wanasema wamethibitisha kuwa shughuli kwenye ufukwe wa Milandore zitafungwa kwa muda wote wa majira ya kiangazi.
Hatua hiyo imewagadhabisha wakazi wa maeneo hayo ya mwambao , ambao wametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mpango wa kuziba barabara ya ardhini kuelekea kwenye ufukwe huo.
Familia hiyo ya kifalme ya Saudi Arabia , ikiongozwa na Mfalme Salman, inamiliki jumba la kifahari ambalo Rita Hayworth alitumia kama mahala pa mapokezi ya wageni wakati wa harusi yake .
Sir Winston Churchill na Elizabeth Taylor walikua miongoni mwa wale waliolitumia kama makazi ya mapumziko.
Wakazi wa eneo hilo wamekasirishwa na shughuli za ukarabati katika eneo hilo, hasa baada ya kuwekwa kwa sakafu kubwa ya saruji kwenye mchanga ulioko ufukweni, zimeleza ripoti za wakazi wa eneo hilo.
Blandine Ackermann, rais wa shirika la wanaharakati wanaolinda mazingira katika maeneo ya Golfe-Juan na Vallauris amesema anapanga kuchukua hatua za kisheria kama ufukwe huo hautaendelea kuwa wazi na kurejeshwa katika hali yake
Maafisa wa kulinda bahari wamesema tayari kuwa chombo chochote hakitaruhusiwa kukaribia eneo hilo kwa takriban mita 300 ndani ya bahari.
Saa 24 Baada Ya Kukamilisha Usajili, Ronaldinho Gaucho
Saa 24 Baada Ya Kukamilisha Usajili, Ronaldinho Gaucho Aanza Kuwachanganya Mashabiki Wa Klabu Atakayoitumikia Msimu Ujao,
Thursday, July 16, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)