Tuesday, July 21, 2015

Nkurunziza anatarajiwa kushinda

Raia wa Burundi wanapiga kura Jumanne hii katika zoezi lililoghubikwa na milio ya risasi na miripuko ya magruneti, huku rais Pierre Nkurunziza akitazamiwa kushinda muhula wa tatu licha ya ukosoaji wa kimataifa.

PICHAZ: HAWA NDIO MASTAA WAKUBWA WA NIGERIA WALIOFUNGA NDOA ZA KIFAHARI DUNIAN 2015

 JAPOKUWA mwaka huu wa 2015 umepita nusu yake ni mengi yametokea katika ulimwengu wa burudani ambapo waburudishaji  wengi walioanza mwaka wakiwa ‘wapweke’ hivi sasa wana wenza wao waliofunga nao ndoa na wanategemea kufanya hivyo kabla mwaka huu haujaisha.
 Mtandao wa Nigeriafilms.com umekuwa ukiweka kumbukumbu na sasa unaweza kuonyesha ndoa za ‘nguvu’ ambazo zimetamba katika nusu ya kwanza ya mwaka 2015. 
Paul Okoye na AnitaIsama . 
Ndoa ya kimila iliwakutanisha Peter, mmoja wa mapacha wa kundi la muziki la Psquare alipomchukua mpenzi wake wa siku nyingi na mama wa mtoto wake, , Anita Isama. Tukio hilo lilifanyika mwezi Januari huko Ikoyi, Nigeria
Peter Okoye na Lola Omotayo-Okoye.
Kama ilivyokuwa kwa kaka yake, mwanamuzaiki  maarufu,  Peter Okoye, na mama wa watoto wake wawili, Lola Omotayo, waliimarisha uhusiano wao kwa kufunga ndoa huko Ikoyi.
Chris Attoh na  Damilola Adegbite.
Wawili hawa walioana siku ya Wapendanao ya Valentine -- Februari 14 – katika ndoa ya kimyakimpya jijini Accra, Ghana ambapo biharusi Damilola Adegbite alikutana na mpenzi wake, mtoto wa mfalme wa kikabila huko Ghana, Chris Attoh, kwenye mahojiano ya kipindi cha televisheni cha Mnet cha Tinsel.
Japokuwa wawili hao wanasema watafunga ndoa nchini Nigeria,  marafiki zao wanasema wana hamu ya kuona hilo linatokea kabla ya kumalizika kwa mwaka 2015.
Gbenro Ajibade na  Osas Ighodaro.
NI dhahiri Gbenro Ajibade bado ana furaha isiyomithilika kwa kumuoa kipenzi chake, Osas Ighodaro, ambaye hadi sasa bado wako kwenye fungate.  Wawili hao walioana Jumamosi ya Julai 4, 2015 jijini New York Marekani.:

Kenyatta: Hatutajadili jinsia moja

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa maswala la mapenzi ya jinsia moja hayajaratibiwa katika mazungumzo baina yake na mgeni wake mashuhuri rais wa Marekani Barack Obama.
Rais Kenyatta aliyasema hayo katika hotuba kwa waandishi wa habari kuhusu ratiba ya rais Obama nchini humo.
Kenyatta alisema kuwa yeye anatarajia kumpokea rais Obama siku ya ijumaa na kuwa
''hilo sio moja kati ya maswala yaliyopangiwa kuzungumziwa''
''Kama wakenya tiaf letu linakabiliwa na changamoto nyingi tu nafikiri tunamaswala ya muhumi zaidi ya kujadiliwa mbali na hilo la mapenzi ya jinsia moja'' alisema rais Kenyatta akijibu swali alilorushiwa na mwanahabari.
Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Kenya.
Kabla ya kujibu maswali ya waandishi wa Habari rais Kenyatta alikuwa ameisifu taifa lake kwa kuwa mwenyeji wa kongamano la wajarsiria mali ''Global Entrepreneurship Summit'' (GES) akisema hii ni mara ya kwanza kwa kongamano hilo kuandaliwa kusini mwa jangwa la sahara.
''Hii ni fursa nzuri na kubwa kwa wajasiria mali wakenya kukutana na kubadilishana mawazo na wenzao wa kimataifa'' alisema Kenyatta.
Vijana wetu bila shaka wameweka kigezo cha ubora katika ujasiria mali na ubunifu hata kuvutia mabwenyenye wa kimataifa wanaotafuta sekta za kuwekeza''aliongezea bwana Uhuru.
Mbali na hayo bwana Kenyatta alikariri kuwa Obama atakuwa mgeni wa serikali ya Kenya wala sio yeye kama rais Uhuru Kenyatta.
Aidha alisema ''swala la iwapo atakutana na naibu wa rais bwana William Ruto licha ya kukabiliwa na mashtaka katika mahakama ya ICC huko Hague halipaswi kuibuka''.
Huku hayo yakijiri, hali ya usalama imeimarishwa vilivyo katika mji wa Nairobi na viunga vyake na hasala maeneo yanayotarajiwa kuwa mwenyeji wa rais Obama.
Helikopta 4 za kijeshi za Marekani zilipaa juu ya mji wa Nairobi na kisha kutua katika chuo kikuu cha Kenyatta lililoko viungani mwa jiji hilo.

Waziri mkuu Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo lake

Waziri mkuu Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo lake la uchaguzi la Katavi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo.Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wengine nafasi.

Ziara ya mfalme wa Saudia Ufaransa yazua Ubishi

 Ubishi umeibuka nchini Ufaransa, baada ya ufukwe maarufu wa bahari wa Riviera kufungwa ilikumruhusu mfalme wa Saudi Arabia na familia yake kujivinjari kwa amani faraghani.
Viongozi wa mji wa Vallauriswametangaza kuwa watafunga sehemu kubwa ya ufukwe huo ilikuhakikisha usalama wa mfalme huyo familia yake na takriban ujumbe wa watu 400.
Familia hiyo ya kifalme, inatarajiwa kuishi katika jumba la kifahari lililoko huko.
Jumba hilo lililowahi wakati mmoja kuwa jumba la mapumziko la Sir Winston Churchill linatarajiwa kuzingirwa na maafisa wa usalama.
Maafisa wa Vallauris iliyoko kwenye mwambao wa Cote d'Azur, kilomita 10 kutoka kwenye ufukwe huo wanasema wamethibitisha kuwa shughuli kwenye ufukwe wa Milandore zitafungwa kwa muda wote wa majira ya kiangazi.

Hatua hiyo imewagadhabisha wakazi wa maeneo hayo ya mwambao , ambao wametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mpango wa kuziba barabara ya ardhini kuelekea kwenye ufukwe huo.
Familia hiyo ya kifalme ya Saudi Arabia , ikiongozwa na Mfalme Salman, inamiliki jumba la kifahari ambalo Rita Hayworth alitumia kama mahala pa mapokezi ya wageni wakati wa harusi yake .
Sir Winston Churchill na Elizabeth Taylor walikua miongoni mwa wale waliolitumia kama makazi ya mapumziko.

Wakazi wa eneo hilo wamekasirishwa na shughuli za ukarabati katika eneo hilo, hasa baada ya kuwekwa kwa sakafu kubwa ya saruji kwenye mchanga ulioko ufukweni, zimeleza ripoti za wakazi wa eneo hilo.
Blandine Ackermann, rais wa shirika la wanaharakati wanaolinda mazingira katika maeneo ya Golfe-Juan na Vallauris amesema anapanga kuchukua hatua za kisheria kama ufukwe huo hautaendelea kuwa wazi na kurejeshwa katika hali yake
Maafisa wa kulinda bahari wamesema tayari kuwa chombo chochote hakitaruhusiwa kukaribia eneo hilo kwa takriban mita 300 ndani ya bahari.

Saa 24 Baada Ya Kukamilisha Usajili, Ronaldinho Gaucho

Saa 24 Baada Ya Kukamilisha Usajili, Ronaldinho Gaucho Aanza Kuwachanganya Mashabiki Wa Klabu Atakayoitumikia Msimu Ujao,

Thursday, July 16, 2015

https://youtu.be/RPRcmt6HSl0

https://youtu.be/RPRcmt6HSl0

Breaking Newzz....ANGALIA MATOKEO YA MTIHANI YA KIDATO CHA SITA (NECTA)

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha sita uliofanyika mwezi wa tano mwaka huu yametoka leo.
-Yametangazwa rasmi na Baraza la Mitihani la Taifa(NECT

Matokeo ya Kidato cha Sita yametangazwa mtandaoni rasmi na Baraza la Mitihani nchini almaarufu kama NECTA. Kuyaona matokeo hayo ingia hapa:

http://necta.go.tz/matokeo/2015/Alevel.htm

Matokeo ya Ualimu 2015 Nayo Yako Hewani


YAANI HUU UCHAFU ULIOFANYIKA KWENYE HII PARTY YA KIBAO KATA BEACH ...NI FULL LAANA.












HATIMAYE ZITTO KABWE AWAUNGANISHA DIAMOND NA ALI KIBA


Ningekuwa mtoto wa magufuli

Ningekuwa mtoto wa magufuli ningeanza kuhamisha mizigo yangu kupeleka ikulu nikawah chumba ambacho dilisha lake linaangalia baharini"""" hayo ni maneno ambayo alikuwa akiyaongea mtoto mmoja huko uswazi katika pitapta zangu

Picha ya Mwaka 1997 ya Monalisa Akiwa Mama Yake ‘Natasha Mamvi’, Yawafurahisha Wengi

Picha ya kitambo ya Staa wa bongo Movies, Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ akiwa na mama yake mzazi ambaye pia ni staa wa Bongo Movies, Susan Lewis ‘Natasha’ aliyowekwa na Monalisa kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa instagram imewafurahisha mashabiki wao wengi na kutupia komenti za kicheko na kuwasuifia kwa jinsi walivyotokelezea .

VAN PERSIE APOKELEWA KWA MADAHA TIMU MPYA

Wakati Bastian Schweinsteiger, Matteo Darmian na Morgan Schneiderlin wakielekea Old Trafford kukamilisha ndoto zao za kujiunga na moja ya vilabu vikibwa duniani, Robin van Persie yeye ameondoka kwenye klabu hiyo.


Mshambuliaji huyo wa kiholanzi ambaye alijiunga na Manchester United mnamo mwaka 2012 akitokea Arsenal kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 24, sasa anaelekea klabu ya Fernabahce.

Mshambuliaji huyo jana alisafiri kwenda Istanbul na alipokelewa kama mfalme na mashabiki wa klabu yake mpya.
Van Persie ambaye aliiwezesha United kushinda ubingwa wa 20, akifunga magoli zaidi ya 20, msimu uliopita alikumbwa na balaa la majeruhi akiishia kufunga magoli 10 tu. “Nimekuja kujiunga na klabu nzuri na kubwa, ni heshima kubwa kwangu.” Alisema Van Persie.



Fenerbahce walithibitisha Alhamisi kwamba wameingia kwenye mazungumzo na United juu ya uhamisho wa ndachi huyo.
Van Persie sasa anaungana na mchezaji mwenzie wa zamani wa United, Luis Nani.



Victor Valdes kuuzwa kwa utovu nidhamu

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema watamuuza mlinda mlango wao Victor Valdes kwa kuwa hafuati filosofia yake.
Van Gaal anasema Victor Valdes alikataa kucheza katika kikosi cha akiba.
Hafuati filosofia yangu. Hakuna nafasi ya mtu kama huyo.
Na kuhusu kumuuza De Gea, Van Gaal anasema, siwezi kusema kitu, yuko vizuri, ni upuuzi kuuliza.

Di Maria kujiunga na PSG

Mchezaji wa Manchester United Angel Di Maria amewaeleza wakuu wa kilabu ya PSG nchini Ufaransa kwamba anataka kujiunga na kilabu hiyo.
Kulingana na gazeti la Le Perisien mazungumzo kati ya vilabu hivyo viwili yanaendelea huku wakidaiwa kukubaliana kwa kitita cha pauni milioni 42.8.
Di Maria amekosa kuichezea Man United katika ziara ya timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu ujao nchini Marekani akidaiwa kupumzika baada ya kushiriki katika kombe la Copa America.

Umri wa kuolewa Uhispania ni miaka 16

Uhispania imepandisha umri unaoruhusiwa kwa wasichana kuolewa hadi kumi na sita.
Hadi sasa wasichana nchini humo wangeruhusiwa kuolewa wakiwa na miaka kumi na nne bora tu wapate ruhusa ya jaji.
Sheria hiyo mpya sasa inanuiwa kupunguza visa vya udhalilishaji wa watoto nchini humo.

Picha ya kwanza kutoka sayari ya Pluto

Picha ya sayari ya Pluto
Picha ya kwanza inaonyesha kwa undani sayari ya Pluto ilivyo imeonyeshwa kwa mara ya kwanza duniani.
Picha hiyo imepigwa na chombo kisicho na binadamu kilichotumwa kwenye safari hiyo ambacho kilisafiri umbali wa kilometa bilion saba na tano.
Chombo hicho jana jumanne kilitua kwenye sayari hiyo .
Katika mkutano na waandishi wa habari katika chuo Kikuu cha Johns Hopkins kilichopo Maryland Marekani, Mkuu wa utafiti wa sayari hiyo Alan Stern hakusita kuonyesha furaha yake.
"Jana ilikuwa ni siku nzuri na ya kipee kwangu, vipi kwenu."
Mkuu huyo wa utafiti - Alan Stern amesema chombo hicho cha anga kimekusanya taarifa nyingi kutoka kwenye sayari hiyo
"Sawa chombo chetu cha New Horizons kimekwenda sasa zaidi ya mile milioni moja.Zaidi ya kilometa moja na nusu upande wa pili wa Pluto, hivyo ndivyo tunavyokwenda kwa haraka tumefikia karibu na sayari hiyo hapo jana asubuhi. Chombo chetu cha anga kipo katika hali nzuri, kinafanya mawasiliano na dunia kwa mara nyingine mara kwa mara kwa masaa kuanzia asubuhi saa 11 na dakika 50. Tayari tumepata data kutoka kwenye vifaa vya kisayansi vipatavyo vitano, na tutatoa taarifa kuhusu matokeo tuliyopata, lakini ukweli ni kwamba tunachunguza kwa undani , kuna mengi." Amesema Alan Stern.

Real Madrid ndio kilabu tajiri duniani
























Real Madrid ndio timu tajiri zaidi kwa mwaka wa tatu mfululizo kulingana na jarida la biashara la Forbes.
Kilabu hiyo ya Uhispania ina thamani ya pauni bilioni 2.08 huku timu ya soka ya Marekani Dallas Cowboys na ile ya New York Yankees zikichukua nafasi ya pili kwa pamoja na thamani ya pauni bilioni 2.04.
Mahasimu wakubwa wa Real Madrid Barcelona wanachukua nafasi ya nne wakiwa na thamani ya pauni bilioni 2.02.
Kilabu ya Manchester United iko katika nafasi ya tano kutoka nafasi ya tatu mwaka uliopita.
Nafasi nyengine zilizosalia katika kumi bora zinachukuliwa na timu za michezo nchini Marekani.
Timu nyengine za ligi ya Uingereza ni Mancity iliopo katika nafasi ya 29 ikiwa na thamani ya pauni milioni 890,Chelsea ikiwa na thamani ya pauni milioni 877 inachukua nafasi ya 31 na Arsenal yenye thamani ya pauni milioni 839 ikiwa katika nafasi ya 36.

Wednesday, July 15, 2015

Timu 6 kukata utepe,CECAFA

Ratiba ya mechi ya mechi za ufunguzi katika michuano ya Kombe la Kagame CECAFA imekwisha kufahamika ambapo jumamosi hii APR ya Rwanda itakwana na Al Shandy ya Sudan majira ya saa nane mchana kwa saa za afrika mashariki.
Mechi ya pili itakuwa kati yaYanga ya Tanzania na Gor Mahia ya Kenya mchezo utakao chezwa saa saa 10 za jioni kwa saa za Afrika mashariki. Muda huo huo KMKM kutoka visiwa vya Karafuu Zanzibar itakuwa na mtihani mkali pia dhidi ya Telecom ya Djibout.
Katika historia ya michuano hiyo,Simba ya Tanzania ndiyo inaongoza kwa kutwaa ubingwa mara nyingi,kwani ni mara sita hadi sasa ikifuatiwa na Yanga huku Gr Mahia ikiwa imetwaa mara tano na APR ya Rwanda mara tatu.

Bodi ya Mikopo ya wanafunzi

Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu imesogeza mbele tarehe ya Mwisho ya kupokea maombi ya mikopo kwa Wanafunzi.
-Tarehe ya Mwisho ya kupokea maombi itakuwa 31 Julai, 2015

EU kuipa Ugiriki mkopo wa dola bilioni 7

Tume ya bara Ulaya imependekeza mkopo wa muda mfupi wa dola bilioni saba nukta saba kwa Ugiriki, huku majadiliano kuhusu madeni ya nchi hiyo yakiendelea.
Utatolewa kupitia mfumo wa hazina maalum ya udhabiti wa kifedha unaohusisha mataifa yote 28 wanachama wa bara Ulaya.
Baadhi ya mataifa wanachama wa EU ambayo hayatumii sarafu ya Euro, kama vile Uingereza yanapinga wazo hilo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa vyama vya kisiasa nchini Burundi vimekubaliana kufanya mazungumzo ili kuafikia makubaliano.

Tuesday, July 14, 2015

Bunge la Rwanda limepiga kura kuruhusu mabadiliko ya Ibara 101

Bunge la Rwanda limepiga kura kuruhusu mabadiliko ya Ibara 101 ya Katiba, kuruhusu muhula wa tatu kwa Rais Paul Kagame mwaka 2017. 

-Awali Wanyarwanda milioni 3.7 walitia sahihi ombi la kumtaka Rais Paul Kagame kugombea muhula wa tatu

Mgombea urais wa UKAWA bado kitendawili

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA vimetangaza rasmi kufikia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA vimetangaza rasmi kufikia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Akitangaza makubaliano hayo mara baada ya kumalizika kwa kikao kirefu kilichokuwa kikijadili mustakabali wa kumpata mgombea urais pamoja na ugawanaji wa majimbo mapya, mwenyekiti mweza wa UKAWA James Mbatia amesema kuwa umoja huo umemteua mgombea ambaye ni chaguo la watanzania.
“Mgombea tutakayemtaja ndiye chaguo la watanzania” Amesema Mbatia
Mbatia amegoma kutaja jina la mgombea aliyepitishwa na umoja huo kwa madai ya anaandaliwa utambulisho maalum utakaoambatana na shamra shamra.
“Tayari jina tunalo lakini tutaliweka hadharani baada ya siku tano au sita hivi, na tutamtoa kwa kimasomaso”
Katika kikao hicho kilichomalizika majira ya saa 3:30 usku kikihusisha wenyeviti wa vyama hivyo pamoja na kamati ya ufundi ya UKAWA, mwenyekiti mwenza wa UKAWA kutoka chama cha wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba hakuweza kuhudhuria.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka CUF, chama hicho kilimuagiza Naibu Katibu Mkuu wa CUF Magdalena Sakaya kuiwakilisha, lakini baadaye Sakaya aliondoka katika kikao hicho bila maelezo yoyote.
Mkurugenzi wa mawasisliano wa chama hicho bwana Abdul Kamaya alipoulizwa kuhusiana na hilo akasema kuwa hakuna mwakilishi yeyote wa CUF aliyekuwepo kikaoni hapo hadi kikao hicho kikimalizika.
Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohamed alipoulizwa kuhusiana na kukosekana kwa Prof Lipumba kikaoni hapo amedai kuwa Prof Lipumba ni mgonjwa, na hali yake ya kiafya haimruhusu kuhudhuria kikao hicho.
“Mwenyekiti wetu ni mgonjwa, alikuwa safarini kutoka Kigoma, amerejea lakini hali yake si nzuri, ameshikwa na Malaria kali sana na miguu pia inamsumbua” Amesema Rajab Mbarouk.
Katika hatua nyingine, afisa habari wa CHADEMA Tumaini Makene aliwaambia waandishi wa habari kuwa tayari vyama hivyo vimekamilisha kazi ya kugawana majimbo mapya 26 kazi iliyofanyika leo katika kikao hicho.

Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza daktari John Magufuli kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa ujao.

Mwanamuziki 50 Cent ajikinga kufilisika

Moja ya wasani maarufu duniani na nyota wa miondoko ya hiphop, rapa 50 Cent , aomba sheria ya kufilisika yenye kifungu cha 11 imlinde na mali zake huko marekani.
Hoja hiyo ilikuja siku chache baada ya mahakama kuamuru rapa huyo alipe dola za kimarekani milioni tano kwa mwanamke aliemshitaki kwakile alichokisema kuwa aliweka video chafu mitandanoni bila ya ridha yake.
Mwanamziki huyo mwenye jina halisi la Curtis James Jackson wa tatu ameuza zaidi ya albamu milioni thelathini duniani kote.